HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

14 April 2011

MANYARA STARS YAONDOKA LEO KWENDA KAMPALA

shaban kado akipokea bendera kutoka kwa iddy kipingu mwenyekiti wa baraza la michezo tanzania
Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 inatarajia kuagwa kesho (Aprili 14 mwaka huu) saa 7 mchana katika ofisi za TFF kabla ya kuondoka saa mbili baadaye kwenda Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya mchujo ya michezo ya Afrika (All Africa Games) itakayochezwa Jumamosi (Aprili 16 mwaka huu)
Msafara wa timu hiyo utakuwa na wachezaji 20 na benchi la ufundi lenye watu sita ukiongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), Hafidh Ally Tahir.
Pia leo mchana (Aprili 13 mwaka huu) timu hiyo imekabidhiwa jumla ya sh. milioni 22 ambazo iliahidiwa endapo ingeitoa Cameroon kwenye michuano ya Olimpiki. Fedha hizo ziliahidiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kampuni ya Simba Trailers.
NSSF kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wake Dk. Ramadhan Dau ilikabidhi sh. milioni 10 wakati Azim Dewji ambaye ni Mkurugenzi wa Simba Trailers alikabidhi sh. milioni 12. Kati ya fedha hizo ilizotoa Simba Trailers, sh. milioni 10 ni kwa ajili ya timu, sh. milioni mbili kwa ajili ya kipa aliyeokoa penalti na wafungaji wa mabao mawili ya U23. U23 imepangiwa kucheza na Nigeria katika raundi ya pili ya michuano ya Olimpiki ambapo mechi ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Juni 4 na 5 mwaka huu.
Wachezaji watakaokuwemo katika msafara huo niShaaban Kado, Juma Abdul, David Luhende, Babu Ally, Shomari Kapombe, Jabir Aziz, Salum Aboubakar, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata, Kigi Makasi, Gharib Mussa, Mbwana Bakari, Idrisa Abdulrahim, Innocent Wambura, Khamis Mcha, Awadh Issa, Amour Suleiman, Himid Mao, Mrisho Ngassa na Salum Telela.

1 comment:

  1. Hey..
    Nice Article, clear and detailed description...
    Thanks a lot for sharing the information.....

    By the way check the latest information about the All Africa Games 2011 here, like events, programs, All Africa Games 2011 Schedule, dates, All Africa Games 2011 Results and more from All Africa Games 2011.

    ReplyDelete

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers