HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

20 December 2012

Rais Kikwete akutana na Mmiliki na viongozi wa Sunderland Ikulu

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mmiliki na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short (kushoto kwa Rais), Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband (kulia kwake), Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Kagasheki, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr Fenella Mukangara, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim pamoja na maafisa wa Bodi ya Utalii bada y mkutano na Rais Ikulu jijijni Dar es salam leo.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi toka kwa mmiliki na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short huku Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband na Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan wakiangalia bada ya mkutano wa na Rais Ikulu jijijni Dar es salam leo.

Uongozi huo wa Sunderlanda umesema kuwa baada ya kukutana na balozi wa Tanzania nchini humo na kuzungumza nae kuhusu swala la uwezekezaji Mwenyekiti wa klabu hiyo ameona bora waje kuonana na Viongozi wakuu wa   nchi hasa baada ya Tanzania kudhamini ligi kuu ya Uingereza kwa kupitisha mabango mbalimbali yahusuyo utalii katika ligi hiyo ,
Aidha Rais kikwete amemsifu balozi wa Tanzania Nchini Uingereza  kwa kazi walioyofanya na Waziri wa utalii Mh kagasheki  kwani wamefanya kazi nzuri zaidi kipindi hiki .

Kwa upande mwingine baadhi ya wachezaji watapa mafunzo ya kwenda sunderland hasa wenye umri mdogo zaidi 

Viongozi hao wa sunderland wamesema kitu kikubwa watakachofanya ni kuendeleza michezo katika sekta ya uongozi na na kutazama namna ya kutoa mafunzo kwa wachezaji na viongozi wa soka hasa katika swala la menejiment ambalo ndilo eneo lenye udhaifu zaidi katika michezo ,
kwa upande mwingine Rais alimwalika Mh Aden Rage mwenyekiti wa klabu ya soka simba ambao zamani walikuwa wakitumia hilo kabla ya kubadili kuitwa simba naibu waziri wa michezo fenela mukangara amesema kuwa hii ni faida ya kwanza  ambayo tanzania inapata baada ya kutangaza katika ligi hiyo na waanaamini fursa zaidi zitajitokeza katika kutangaza katika ligi hyo .

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short huku Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband na Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan Ikulu jijijni Dar es salam leo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short, Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband, Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Kagasheki, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr Fenella Mukangara, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim pamoja na maafisa wa Bodi ya Utalii bada y mkutano na Rais Ikulu jijijni Dar es salam leo.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers