HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

4 April 2013

SIASA INAVYODIDIMIZA MICHEZO MASHULENI !!!!

 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj-hW9eeQkdPAYTHUUSIeiDjTHCXuApO_FAk2u4t0Ge4LnxrfMe-o3LZV_VuxXB7awPwjCAyrMXbaqIgf_PJ18V9qcwIRrH-IWcxEcWOOAAs0Ds6PFKn84JkanqHs2Ss9C3I11wbR-88C4/s1600/PTDC0029.JPG 
 
HABARI mpenzi msomaji wangu. Leo imekuwa bahati kwani wiki hii niliamua kutembelea Shule ya Msingi Mtakuja, iliyopo Kunduchi Mtongani, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kuiona shule hiyo niliyosoma miaka kumi na tatu iliyopita, inaendeleaje.

Nilikwenda kutazama jinsi sera ya michezo mashuleni inavyofanya kazi, ambapo nilikutana na mengi ambayo yanasikitisha, lakini wakati mwingine inabidi ucheke - si kwa furaha, bali cheko la masikitiko ndani yake.
Jambo la kwanza niliingia kwenye darasa ambalo halikuwa na mwalimu, ambalo lilikuwa lina makelele utafikiri sokoni Kariakoo. Kama ilivyo ada, ratiba za vipindi hupachikwa nyuma ya mlango, somo la mchezo kwenye ratiba lipo na kwa bahati kipindi kilichokuwa kinafuata ni cha michezo.
http://4.bp.blogspot.com/_b5srj3d_Ppw/St8RocStHjI/AAAAAAAABG8/IlUVlTmcfao/s320/wanafunzieeeh%5B1%5D.jpg
Nilitoka nje na kukaa kwenye bustani, kusubiri nione kama mwalimu ataingia huku nikizungumza na wanafaunzi hasa mambo ya michezo, wengi wao wakiwa hawajui kabisa kuhusu UMISHUMTA na UMISETA, ambayo ni michezo maarufu ya kubuia vipaji shule za msingi na sekondari kwa Tanzania.
Lakini michezo hiyo imerudi mashuleni kinadharia na si kwa kivitendo. Siasa imekuwa tatizo kubwa katika tasnia ya michezo mashuleni na kwingineko, kutokana na ukweli kuwa, viongozi wengi wamekuwa wakiongoza vyama au klabu na kisha kuziacha na kukimbilia siasa.
Hapa simsemi Katibu wangu wa zamani wa TFF, Fredrick Mwakarebela, ambaye binafsi kwangu ni mwadilifu. Katika kukaa na wanafunzi wale nilikuwa nataka kuelewa uwelewa wao wa michezo, siku hiyo kulikuwa na darasa la nne, sita na saba, na kwa muda niliozungumza nao mpaka namaliza, sikuona mwalimu yeyote wa somo hilo akiingia darasani, nikahisi labda siku hiyo hakuwapo.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiGkVWtB7SHRGnZdueWtbM-NUAF-dMiQ26B4_VJfi_Sub212LPIUgz1zE2grvYAw41p-sfVNA1fbl1xbL6fe4HGk1x0q_Wnv8K_-0ur0gmCrR4ZGOfCGn8k6OZ24GStrvsokR-ZrlhrfxXt/s1600/TUIKUZE+MICHEZO.jpg
Wanafunzi wakaniambia somo la michezo huwa tunafanya mtihani tu, sikushangaa sana kwani ndio mfumo ambao hata mimi ninayeandika makala hii nilipitia. Lakini wakati huo sera ya michezo ilifutwa kwa kigezo kuwa wanafunzi wanafeli sana mashuleni.
Kuna mwalimu ambaye sitamtaja jina, aliniambia serikali haijaleta mwalimu wa michezo na hata mipira, ambayo mashuleni ipo ya wanafunzi wenyewe ambao wanahusudu soka na huja shule na mipira waliyonunuliwa na baba zao nyumbani.
Wanafunzi walio wengi, walionyesha uelewa kwa kufahamu kidogo katika mpira wa miguu na kujua baadhi ya nafasi kiwanjani kama kipa, beki, mshambuliaji, refa na mashabiki idadi ya wachezaji dimbani, basi.

Hii ni picha ambayo ukiitazama utaona dhahiri kuwa sera ya michezo mashuleni imerudi kwa maandishi ya viongozi, lakini haijarudi rasmi kivitendo na kwa nilichokigundua, inaonyesha dhahiri Tanzania bado tuna safari ndefu kuelekea mafanikio, kwani yapo baadhi ya mambo muhimu tunayafanya kwa siasa tena za uongo wa hali ya juu.
Hivi kweli serikali imerejesha michezo mashuleni, au ndio imetoa taa ya kijani kwa wanafunzi kucheza bila mpangilio? 

Jambo kuu ninalohisi michezo imerudi kwa utashi wa kisiasa wanafunzi wengi ambao huanza darasa la kwanza umri wao ni miaka saba umri sahihi kabisa wa kumfundisha michezo.
Lakini wengi wa wanafunzi hawa ndio wa kwanza kucheza mpira kwa kutumia mashine za kompyuta ‘play station’.
Kubwa kati ya yote ambalo nasimamia mada yangu ya msingi ni kuwa, kuonyesha kwamba michezo imejaa siasa, wakati wa uchaguzi viongozi wote wa nchi hii waliwahi kuweka ligi za soka huku zikitumia majina ya binafsi na kipindi hicho, huonyesha moyo thabiti wa kupenda na kundeleza michezo ili tu waingie bungeni.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhb54SH-wwDYOKhfCCPr2Iz8QbL5NfdyR4QoxFxERBiBssin8_6pBvjUuTZRohU5pULLt39LxjLl1-urd1K54-4TuE3XZnylyTxhbvxtldUvEIfbK4Ux0tGhmkSuZUgZJ-A8oQIwH3s8T3r/s1600/mwinyi1.jpg
Wakifanikiwa, wanaanza kuulizia posho, hata kusahau walichotumwa na wananchi, ukitazama hata bajeti ya michezo inatosha kulipia mishahara tu ya Ofisa Utamaduni, na timu za taifa zinapokwenda nje kushiriki michuano ya kimataifa, hupewa bendera na nasaha nyingi kana kwamba walisaidia maandalizi.
Wachezaji wengi wa michezo mingi Tanzania, huwa wanacheza michezo hiyo kwa juhudi binafsi na makocha hukutana nao wakati wakicheza kwenye klabu kubwa.
Kwa mfumo huu ambao shule haina mwalimu wa michezo, mipira, viwanja na kutokutilia maanani michezo, ni ndoto kabisa kuendeleza michezo. Tatizo kubwa tumekuwa tukitaka kufanikisha mambo bila kufuata misingi ya michezo, lakini tumekuwa hodari kusifia ufundi wa nchi za wenzetu kuwa zinafuata maandalizi sahihi ya michezo.

Sisi siasa imechukua nafasi nyingi zaidi kila sekta, si michezo tu, hata kwa mambo mengine. Nilipokuwa shule, mwalimu wangu wa Jiografia alikuwa akifundisha na somo la Sanaa. Tulikuwa tukichora, huku tunafundishwa muziki, japokuwa kinanda kilikuwa kinachorwa ubaoni, lakini leo ukitaka muziki nenda Basata ukafundishwe kozi na King Makusa na Juma Ubao.
Siasa imeharibu mifumo mingi ya uendelezaji soka, binafsi namsimfu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, katika uongozi wake alijenga viwanja vingi vya soka, ambavyo zama za sasa vinatia kichefuchefu hata kuviona. Siasa hizo!

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers