HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

13 November 2014

MBONA IMEKUWA NONGWA KUHAMIA KARUME(MALINZI SIKIZA SAUTI)





Raisi wa shiriksiho als oka nchini TFF Jamal Malinzi amesema suala la kurejesha ofisi za shiriksiho hilo maeneo ya Karume jijini Dar es salaam kama walivyoshauriwa na FIFA, huenda likachukua muda kutokana na ukarabati ambao unatakiwa kufanywa kwenye ofisi hizo.

Malinzi amesema haoni sababu ya kuharakisha kurejea katika ofisi za zamani za TFF, ili hali FIFA walitoa ahadi ya kusaidia sehemu ya ukarabati wa ofisi hizo, hivyo amewataka wadau wa soka kuwa na subra na jambo hilo japo kuna wengine wanaendelea kulivalia njuga kwa sababu zao binafsi.

Amesema anaamini wapo wanaotamani kuona ofisi za TFF zikirejea Karume kwa malengo mazuri, na pia wapo baadhi ya wadau wa soka nchini ambao wanashinikiza kwa minajili ya kutaka uongozi wake uonekane kama ulikurupuka kuzihamisha ofisi hizo na kuzipeleka kwenye jingo la PPF Tower.



Wakati huo huo Jamal Malinzi akazungumzia sakata la Frank Domayo kusajiliwa na Azam FC, akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Tanzania huko mkoani Mbeya miezi sita iliyopita, hatu ambayo ilimfanya kuunda kamati iliyokuwa inaongozwa na Wakili Wilson Ogunde kuchunguza kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kina.



No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers